JALI AFYA AFYA YAKO :VYAKULA VINAVYOONDOA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI-2
WIKI
iliyopita tulianza makala haya kwa kuangalia aina mbalimbali za matunda
yanayoweza kutibu matatizo mbalimbali yanayowahusu wanawake wakati wa
siku zao (menstruation period). Miongoni mwa matunda hayo ni pamoja na
papai bichi lakini lililokomaa ambalo limeelezwa na wataalamu wetu kuwa
na uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya kipindi cha
hedhi kutokuwa na maumivu.
Aidha,
katika kutibu matatizo hayo, pia kuna mitishamba kadhaa inayoweza
kutibu matatizo ya hedhi kwa wepesi na bila kuwa na madhara yoyote
kiafya, waganga wa jadi mahiri wanaijua miti hiyo.
Katika
suala hili, ili wanawake kujiepusha na kupatwa na matatizo ya maumivu,
kutokwa damu kwa wingi kusiko kawaida, kuchelewa kuona siku zao na
matatizo mengine kama yalivyoainishwa wiki iliyopita, wanashauriwa
kuzingatia suala la lishe. Wanapaswa kujua vyakula gani wale na vipi
wasile ili kujiwekea kinga ya kudumu dhidi ya tatizo hili.
LISHE YA KUDHIBITI MATATIZO YA HEDHI
Matatizo
mbalimbali yanayohusiana na hedhi, yanaweza kudhibitiwa na hatimaye
kutokomezwa kabisa kwa kutibu mfumo mzima wa mwili, ili kuondoa sumu
iliyojilimbikiza katika mwili wa mgonjwa kwa kipindi cha muda mrefu,
sumu ambayo imegeuka na kuwa chanzo cha matatizo yanayojitokeza wakati
wa hedhi.
Mfumo
mzima wa mwili unapokuwa umezingirwa na sumu (toxins), ndiyo huwa
chanzo cha matatizo mbalimbali, yakiwemo hayo yanayojitokeza kwa
wanawake wakati wa hedhi na dawa pekee katika hili ni kuondoa sumu hizo
mwilini kwa njia ya lishe.
Ili
kuondoa uchafu huo mwilini, mgonjwa anatakiwa kuanza mpango maalum wa
kula matunda na mbogamboga pekee, kutwa mara tatu kwa muda wa siku tano
mfululizo. Katika siku hizo anachokuwa anakula ni matunda, juisi za
matunda na mboga mbalimbali pamoja na maji, kila wakati wa kula
unapowadia.
Hii
ina maana kwamba mlo wa mtu huyu, katika kipindi cha siku hizo tano,
utakuwa vyakula vilivyotajwa hapo juu, kuanzia asubuhi, mchana na jioni,
katika kipindi hicho, matunda, mboga na juisi anazokula zitakuwa
zinafanya kitu kinachoitwa kitaalamu kama ‘detoxification’, yaani
uondoshaji wa sumu mwilini kwa njia ya asili aliyotuumba nayo Muumba.
Hata
hivyo, kwa wale wanawake ambao ni wembamba sana, ambao pengine katika
kipindi cha funga hiyo ya matunda wanaweza kupoteza uzito sana, wamepewa
ahueni ama ruhusa ya kunywa glasi ya maziwa fresh sambamba na mlo wao
wa matunda. Hii ni kwa sababu ya kuepuka kupoteza uzito kuliko kawaida.
SAFISHA TUMBO KWA ENEMA
Kama
kweli unataka kuondoa sumu mwilini kwa ukamilifu na mwili wako kuwa
safi na huru wa aina zote za matatizo ya kiafya, katika kipindi cha
funga ya matunda na juisi, fanya ENEMA ya maji ya uvuguvugu ili
kusafisha utumbo mpana na kuwa safi. Enema ni njia ya asili ya kusafisha
utumbo mpana kwa kuingiza maji tumboni kupitia njia ya haja kubwa na
kutoa uchafu wote. (rejea makala zangu za nyuma kuhusu Enema).
UFUATE MLO KAMILI
Baada
ya kumaliza siku tano za funga ya juisi na matunda, mtu mwenye kufanya
zoezi hili atatakiwa kuzingatia ulaji wa mlo kamili utakaotilia maanani
matunda, mboga za majani, vyakula vya nafaka (mahindi, mtama, ulezi n.k)
na nafaka zinazoshauriwa ni zile ambazo hazijakobolewa na kuondolewa
viini lishe (wholegrain). Waepuke kula vyakula vitokanavyo na unga
mweupe, ikiwemo mikate myeupe, sukari, vitu vitamu (confectioneries),
vyakula vya kwenye makopo. Aidha, mtu huyu anashauriwa kuepuka kunywa
chai iliyowekwa majani mengi au kahawa iliyowekwa kahawa nyingi.
UVUTAJI SIGARA UKOME
Kwa
wale akina mama wenye matatizo wakati wa siku zao na ambao wameamua
kuingia katika mpango huu wa kusafisha mwili, hawana budi kuachana
kabisa na uvutaji sigara ili kufanikisha zoezi zima la kusafisha mwili
kwa njia iliyoielezwa hapo juu. Kwa ujumla uvutaji sigara ni mbaya kwa
afya ya binadamu.
Tuonane tena wiki ijayo kwa makala nyingine.
Habari kwa hisani ya GPL
0 comments: